Monday 2 February 2015

HIVI NDIVYO VIJANA WA TULIVYOFUNGA MWAKA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA



Katika kufunga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 taasisi ya YWCA MBEYA kupitia WAJIBIKA PROJECT MBEYA na vijana wa mkoa wa Mbeya kiujumla huku tukishirikiana na Redio HIGHLANDS FM,leo tumeungana katika matukio makuu matatu

1.Kufanya usafi wa mazingira katika hospitali
2.kutoa vifaa vya usafi
3.Ugawaji wa vifaa kwa wagonjwa katika hospitali ya rufaa Mbeya
Tunawashukuruni sana wote ambao tumeshirikiana kuumaliza mwaka 2014, kwa namna moja au nyingine kwa kuweza kufanikisha tukio zima hili la kuwafariji na kuwathamini wenye mahitaji


                            Eneo la kutupa taka baada ya shughuri ya ufagiaji
              Muuguzi wa zamu akitoa maelekezo kwa vijana tuliofika eneo la hospitali
              Viongozi kutoka HIGHLANDS FM wakishiliki kwa pamoja usafi hospitalini




                Project officer wa YWCA WAJIBIKA PROJECT MBEYA
               


     KARIBU SANA KUSHIRIKIANA NASI KWA SIMU 0764761900 au 0715850113

Friday 19 December 2014

MAFUNZO YA UFUATILIAJI WA RASILIMALI ZA UMMA, KWA VIJANA MKOANI MBEYA

WAJIBIKA PROJECT MBEYA, huu ni mradi unaofanya kazi na YWCA MBEYA kwa usimamizi wa YWCA TANZANIA, kwa siku tatu za tunaendesha mafunzo ya UFUATILIAJI WA RASILIMALI ZA UMMA, ambayo yanahusisha vijana kutoka maeneo tofauti ya mkoa wa Mbeya
maeneo ya IFIGA, UYOLE, ITENDE, NSALAGA, na ILOMBA,

Ambao kwa pamoja wataweza kujua namna ya kufanya ufuatiliaji wa rasilimali za umma, na kuwa msaada katika jamii zao
                                              Darasa la mafunzo wakisikiliza
                         Lawrence Chuma,kutoka Dar es salaam akitoka mafunzo




Tuesday 11 November 2014

HIVI NDIVYO TULIVYOFANYA TUKIO LA MAZINGIRA JIJI LA MBEYA

YWCA WAJIBIKA PROJECT MBEYA, huu ni mradi unaosimami na YWCA TANZANIA kwa kwa ufadhili wa KFUK KFUM YA NORWARY ambao kwa pamoja katika mkoa wa Mbeya unasimamiwa na YWCA MBEYA ukiwa unatekeleza mambo makuu manne ambayo ni utoaji elimu ya VICOBA(village community bank) na pia UJASIRIAMALI, MAZINGIRA, PETS(public expenduture trucking system)

katika kufanya tukio la kimazingira tumeweza kuungana na vijana wa jiji la MBEYA katika
UPANDAJI MITI
UPAKAJI RANGI
ELIMU YA MAZINGIRA
MICHEZO KUHAMASISHA MAZINGIRA

Tukio la upakaji wa rangi lilifanyika katika shule ya mapinduzi ambapo na upandaji miti ukafanyika, ndipo vijana wakatembelea ofisi zetu YWCA MBEYA.

Baada ya kumaliza katika ofisi ya YWCA vijana tukaelekea viwanja vya shule ya msingi Nzovwe kupanda miti katika shule ya JITEGEMEE na NZOVWE,ndipo tukio zima la utoaji elimu na kushiriki michezo mbalimbali ikaanza

JIONEEE MATUKIO YA KUTOSHA YA VIJANA WA JIJI LA MBEYA NA MRADI WA WAJIBIKA MBEYA




     Elly Bonke, Eliud Samweli, Isah Nyambeke, pamoja na Brown wakikusanya miti bustani
                            CLIMATE JUSTICE, STOP POVERTY
                                        wotee tukishirikiana tunaweza kubadilisha dunia
   Ezekia akifundisha wengine namna ya kupaka rangi madirishani yaani ilikuwa kufundishana tuu
 Unaona hapa tutapaka kwa dakika 30, tunaelekea viwanjani, umeonaeeee
                               Tutajua tuu kupaka rangi kwa ajili ya jamii yetu
          Wakina mama nao walikuwa pamoja kufanikisha shughuli nzima hiii
                                    Vijana kutoka dogodogo arts group wakiwa kazini
                Project officer wa mradi wa WAJIBIKA PROJECT MBEYA akipaka rangi
                    Tukamaliza mapinduzi ikaanza safari ya kwenda viwanja vya nzovwe
                                          afisa mazingira wa JIJI la Mbeya akitoa elimu kwa wananchi
 Mkurugenzi wa T-MOTIONS akitoa maelekezo namna vijana wanavyoweza kutumia fursa





Team ya kwanza ikawepo BOMBA FM na Team ya pili ROCK FM kuzungumzia masuala ya mazingira kiujumla katika jamiii
                                            Jengo la shule baada ya kupakwa rangi likionekana vyema

                         Afisa afya akipanda mti katika shule ya JITEGEMEE
                    Project office akipanda mti kwa kuhamasisha utunzaji mazingira