Monday 15 September 2014

YWCA- WAJIBIKA CLUB 2, YAFUNGULIWA SEKONDARI YA NZONDAHAKI JIJI MBEYA

WAJIBIKA PROJECT MBEYA:  yafanya ufunguzi wa club ya mazingira katika shule ya sekondari Nzondahaki ambapo wanafunzi wakiongozana na mwalimu wao wa mazingira, walienda kutembelea bustani ya jiji  ya Mbeya, Ambapo walijifunza namna ya upandaji na utunzaji wa mazingira,wakiongozwa na programu officer wa mradi wa wajibika DEBORAH NJULUMI ,pamoja na katibu mama TABITHA BUGHALI,

Na waliwezwa kufundishwa kwa  undani na mkufunzi wa masuala ya mazingira ndugu OMARY MGALLA

                        Haya ndiyo matukio katika ziara ya kujifunza kwa vitendo wanafunzi hawa

                                             WAJIBIKA CLUB 2
                                            Wanaclub wakizidi kujifunza kwa vitendo




Sunday 7 September 2014

HII NDIYO TUKIO LA VIJANA JIJINI MBEYA LILIVYOFANA,

MBEYA YOUTH EVENT 2014, hili ni tukio lililounganisha vijana wa jiji la mbeya katika kupanda MLIMA LOLEZA siku ya tarehe 6/9/2014, hiii ni sehemu ya kwanza ya matukio katika tukio hili ambalo lilihusisha vijana kutoka ndani ya Mbeya na nje ya Mbeya,

Tukio hili ambalo lilisimamiwa na kuasisiwa na kikundi cha MLIMANI YOUTH GROUP ambapo kwa sasa tukio hili litakuwa likitambuliwa kama MBEYA YOUTH EVENT ambapo kila mwaka litakuwa likiadhimishwa katika jiji la Mbeya kama mwaka huu linavyotambuliwa kwa jina la MBEYA YOUTH EVENT 2014

katika kufanikisha tukio hili ambalo kwa sasa ni tukio la vijana taasisi mbalimbali zimehusika kufanikisha kama kampuni ya uchukua video ya T-MOTION, blog ya MBEYA HOME OF TOURISM,  asasi ya YWCA, YMCA, VIJANA MBEYA, FRESOWE,SKAUTI MBEYA,MBEYA LIVING LAB,upigaji picha na EGY BUSINESS SOLUTION,na kwaudhamini wa WAJIBIKA PROJECT MBEYA kubwa zaidi ni vijana wote waliotoka katika sehemu mbalimbali hili ni tukio lenu na kwa pamoja lione ni la kwako na ujipange kwa MBEYA YOUTH EVENT 2015, idadi ya vijana 79 wameshiriki tukio hili

Kazi ikaanza sasa ya kupanda na kauli mbiu "NITASIMAMA, NITATETEA, KIZAZI KIPYA CHA VIJANA UTHUBUTU UNAANZIA NYUMBANI"



                                 Safari ndipo ilipoanza eneo la RETCO katikati ya jiji la mbeya

                                              njiani vijana wa jiji la mbeya wakiicha rami
                                   kwa pamoja vijana wakigawana matunda na kila mtu alipata
                                                    polepole safari inaendelea hapo

                                 mwanzoni tuu mlima kila mshiriki ana hali ya kufika mwisho


            wanasema unavyopanda mlima uchangamfu ni lazima wakina kaka wakitafakari jambo
         mkurugenzi wa T-MOTIONS (ROBERT ELIAH) kwa nyuma na dada BUPE MLABWA
                                   Team ya vijana kutoka MBEYA HOME OF TOURISM
                                         Iliruhusiwa kuimba nyimbo ili mradi tuuu ufike mwisho
                                                        rahaaaaaaaaaaaa
                                                 hawa nao mlima na mapozi kibao ya picha
                    Team MAVUVUZELA kutoka MLIMANI YOUTH GROUP, hawatasaulika hawa
sehemu ya kwanza inaishia hapa msalabani ,jiandae kujifunza mengi kutoka kwa vijana wa jiji la mbeya
NB:
KWA TAASISI, MTU YEYOTE UNAEWEZA KUTUSAIDIA KWA AINA YOYOTE  KUTOA MAONI, USHAURI, UDHAMINI, ILI KUENDELEZA TUKIO HILI KWANI TUNAHITAJI KULIWEKA KATIKA JARIDA, DVD,VIPEPERUSHI, NA NAMNA MBALIMBALI TUNAKUHITAJI , ILI LIWE BORA ZAIDI
Mawasiliano:email; MBEYAYOUTHEVENT2014@GMAIL.COM simu:ELLY BONKE 0764761900

Tuesday 2 September 2014

WAJIBIKA ENVIRONMENT CLUB 1,YAFUNGULIWA MBEYA KATIKA SHULE YA MAPINDUZI

WAJIBIKA mpango huu unajulikana kama harakati za vijana katika uwajibikaji kiuchumi na kimazingira ili kuleta maendeleo endelevu, mradi huu unaosimamiwa na YWCA TANZANIA,YWCA MBEYA kwa ufadhili wa Y GLOBAL KFUK ambao umelenga katika humasisha vijana kuwa na uthubutu katika mambo mbalimbali,
WAJIBIKA CLUB 1,hili ndilo jina la club katika shule ya msingi mapinduzi iliyo katika jiji la mbeya ambapo mradi wa wajibika utakuwa ukifanya kazi hapo shuleni
                                             mwalimu wa shule akifungua mafunzo katika CLUB


                                       wanaclub ya mazingira wakijadiri mambo mbalimbali

mwandishi wa habari na mkufunzi wa mazingira FESTO SIKAGONAMO akisisitiza jambo



                        walimu na wanafunzi wote katika kujifunza kufahamu kuhusiana na MAZINGIRA,
                                                viongozi wa WAJIBIKA CLUB 1
                        DEBORA NJULUMI(program officer) akiwa na wanachama wa club
shughuli ndiyo kwanza imeanza vijana wana moyo wa kujitolea na kufanya kazi, mazingira ni yetu sote